Michezo

Neymar na mchezaji mwenzake wa Barcelona wazichapa mazoezini (+Video)

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, Neymar Jr leo asubuhi amejikuta akitengeneza vichwa vya habari duniani baada ya kupigana na kinda wa Barcelona, Nelson Semedo wakiwa mazoezini nchini Marekani.

Neymar Jr katikati akizinguana na Nelson Semedo

Kwa mujibu wa Gazeti la Marca taarifa zinasema Neymar alichezewa rafu na Nelson Semedo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Benfica kitu ambacho alikichukulia kama amefanyiwa makusudi na ndipo akaanza kuvutana na kuanza kurushiana makonde.

Kwenye video iliyotolewa na mtandao wa Daily Mail inaonesha Neymar akionekana mwenye hasira kwani licha ya kuamuliwa na Javier Mascherano aliendelea kumfuata Nelson ili wazichape.

Hata hivyo ugomvi huo uliisha ingawaje Neymar alivua nguo za mazoezi na kurudi chumbani kwake huku akiwaacha wenzake wakifanya mazoezi.

Tayari kumeanza minong’ono kuwa kitendo hicho huenda kikawa kama chanzo cha yeye kuihama klabu hiyo baada ya tetesi za kuwindwa na matajiri wa ufaransa, PSG.

Neymar akitoa nguo za mazoezi na kuondoka uwanjani

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents