HabariUncategorized

Mganga Mkuu Temeke atoa kilio chake kwa wananchi juu ya wodi ya akina mama

Diwani wa viti maalum Temeke, Mwanakomba Mwinyimkuu (kushoto) akimkabidhi msaada, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temete, Dr. Amaani K. Malima

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dr Amaani K.Malima amewaomba watanzania kujitokeza kusaidia baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo ya vifaa vya upasuaji katika wodi mpya iliyojengwa hivi karibuni.

Amesema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam muda mchache baada ya kukabidhiwa msaada wa magodoro, mashuka na sabuni kutoka kwa madiwani wawili wa viti maalum kutoka wiliayani humo.

Akingumza na waandishi wa habari akiwa hospitali hapo muda mchache baada ya kukabidhiwa, Dr Amaani alisema msaada huyo utaweza kusaidia kutatua baadhi ya changamoto ambas zinaikabili wodi hiyo.

“Kwa niaba ya hospitali nawashukuru sana madiwani wetu, Mwana Kombo Mwinyimkuu na mstahiki Meya Temeke Abdalah Chaurembo kwa kutoa magodoro na shuka pamoja na sabuni ninaamini zitawafikia walengwa ambao ni akina mama na watoto na nina amini utawasaidia sana kwa sababu ni moja kati ya makundi hapa hospitalini kwetu ambayo yana changamoto nyingi,” alisema Dk. Amaani.

Aliongeza,“Lakini changamoto nyingine tuliyonayo ni vitendendea kazi kwahiyo tunaomba wadau wote wenye chochote kitu atusaidie ili tuweze kuboresha uduma zetu. Pia hapa tuna ujenzi unaendelea, tunaukarabati wa majengo unaendelea kwahiyo tungeomba wadau watusaidie hasa kwenye uchakavu wa majengo na vitendeoa kazi. Mahitaji makubwa sasa hivi ni upande wa akina mama, kuna maabara ya akina mama ambayo tayari tumeshatenga jengo lakini changomoto inakuja kwenye vifaa,”

Kwa wa upande wa diwani wa viti maalumu Temeke, Mwana Kombo Mwinyimkuu ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huyo, amesema wameamua kutoa msaada huo ili kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili hospitali hiyo huku akiwataka wadau wengine kujitokeza ikuboresha huduma hospitali hapo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents