Burudani

Wema Sepetu ataweza kuingiza hadi shilingi bilioni 1 kila mwezi kupitia app yake, huu ndio mchanganuo wake

Wema Sepetu amezindua rasmi app yake, WS, kwenye jukwaa la app la simu za Android, Google Playstore.

App yake inapatikana bure kabisa. Ukishainstall, itakuomba usign-up kwa kutumia akaunti yako ya Gmail. Basically, app yake ipo kwaajili ya yeye kuwasiliana na mashabiki wake, kila siku. Anachofanya, ni kuandika mambo mbalimbali kuhusu yeye binafsi kama fashion, muziki, filamu, na hata mahusiano.

Kwa mfano ametumia app hiyo kuwafahamisha mashabiki wake kuhusu kuwepo kwenye orodha ya mastaa walioitwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaohusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Kwenye app hiyo hadi sasa pia, ameweka pia video/audio akizungumzia tattoo zake, timu za mitandaoni, filamu tatu anazozipenda, gharama za nywele zake, nyimbo 3 za Diamond (ex wake) anazozipenda na vingine.
Haya ni mambo ambayo mashabiki wake wanavutia sana kumsikia akiyasema.

Awali, aliweza kuwapa taarifa hizi kupitia akaunti yake ya Instagram au kupitia interview anazofanyiwa, lakini sasa wayatapata kupitia app yake. Tofauti sasa ni kwamba, taarifa hizi mashabiki hawatazipata bure, watalazimika kuzilipitia.

Gharama yake hata hivyo, ni pesa ya madafu kabisa. Mfumo wa malipo ni wa subscription, kama ambavyo huduma za kustream muziki kama Tidal au Spotify hufanya. Shabiki ana option kadhaa rahisi tu, kulipia kwa mwezi, ambayo gharama ni shilingi 1,000 tu (mimi nimejiunga na hiyo), miezi mitatu 2,500 na pia kuna option ya miezi sita hadi mwaka mzima ambayo inaenda ikipungua kwa kadri unavyonunua kifurushi cha muda mrefu.

Wale ambao wamesubscribe, watakuwa na access ya kupata habari na matukio exclusive ya Wema, ambayo huwezi kuyapata kokote, hata kwenye akaunti za mitandao ya kijamii. Kila kitu ambacho atapenda kukisema sasa, atakuwa akikiweka kwenye app yake, na ni subscribers wake pekee watakuwa na access nazo. Kuna option kibao za kulipia kuanzia M-Pesa, Tigo Pesa hadi visa, na hivyo kuwa app inayoweza kuingiza fedha dunia nzima. Kwa kutengeneza hamu zaidi ya watu kudownload app yake, huenda Wema akaanza kuadimika sasa kwenye interview za redio, TV au blog. Ubuyu wote atauweka kwenye app yake.

Sasa hebu tupige hesabu ya kiasi anachoweza kuingiza ndani ya mwezi mmoja. Well, app bado ni mpya na watu ndio wanazidi kuifahamu sasa, na idadi ya watu wanaoidownload muda huu ni kubwa. Rate yake ya ukuaji ni kubwa sana hivyo kuna uwezekano kuwa ndani ya mwezi mmoja, akapata zaidi ya watu 5,000. Kama watu hawa wote watachagua kujiunga kwa kifurushi cha mwezi cha shilingi 1,000, atakuwa ameingiza, shilingi milioni 5.

Pindi app ikichanganya ikawa na watumiaji laki moja, ataingiza shilingi milioni 100 kwa mwezi. Na pale ambapo app itafikisha subscribers milioni moja, kwa kila mwezi atakuwa na uwezo wa kuingiza 1,000,000,000 (shilingi bilioni 1). Ni namba kubwa kuifikia, lakini kwa umaarufu wake, ndani ya miaka kadhaa, ataweza kufikisha.

Bila kusahau kuwa, watu milioni 1 ni nusu ya followers wake zaidi ya milioni 2.5 kwenye Instagram, kwahiyo inawezekana. Na hapo yapasa kuzingatiwa kuwa takwimu za TCRA kuwa hadi mwishoni mwa mwaka 2015, watumiaji wa internet nchini walikuwa ni zaidi ya milioni 17 na wengi wakiipata kupitia smartphone. Kuna uwezekano kwa sasa wamefikia zaidi ya milioni 20, hivyo unaongelea idadi kubwa ya subscribers ambao Wema ataweza kuwavutia kwenye app yake.

Pesa ya subscription, sio pekee atakayokuwa akiingiza. Pindi app yake itakapopata umaarufu, ataweza kuvutia matangazo kutoka google wenyewe ama kutoka kwenye makampuni moja kwa moja na kumlipa fedha nyingi kutangaza bidhaa zao.

Kwa sababu Wema ni mtu maarufu na fan base yake ni kubwa, ana uwezo wa kuwa na content nyingi za kuvutia kwa miaka mingi ambazo mashabiki wake watafurahia kuziona kwenye app. Ana mengi anayoweza kufanya, ikiwemo kuweza kutoa hata series fupi fupi ambazo zitapatikana exclusively kwenye app yake, simulizi za uhusiano wake na mastaa kama Diamond, marehemu Kanumba, Idris Sultan, TID, Mr Blue, Chaz Baba na maisha yake mengine.

Haya yote, ni mambo ambayo mashabiki wake huwa na hamu kubwa ya kuyajua na wako tayari kulipa kiasi chochote ili kupata. Na kwa kutoa app, Wema Sepetu amegundua njia rahisi zaidi ya kufikisha content yake na yeye mwenyewe kutengeneza fedha za kutosha…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents