Michezo

Wenger: Mjadala kunihusu hatima yangu katika klabu “Umeanza kuwa Upuuzi”

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema mjadala unaotokea kila mara kuhusu hatima yake katika klabu hiyo “umeanza kuwa upuuzi”.

3227FEBB00000578-0-image-a-2_1457908423810

Wenger alikuwa akizungumza baada ya Gunners kutolewa katika michuano ya Kombe la FA kwa kufungwa 2-1 na Watford katika mchezo wa robofainali.

Arsenal wameshinda mechi moja pekee kati ya saba walizocheza hivi karibuni.

“Mechi inayofuata huwa mtihani tayari na kila mara unageuzwa kuwa mada ya mjadala. Umeanza kuwa upuuzi,” alisema Wenger.

Arsenal watakutana na Barcelona Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano na wanakabiliwa na mtihani mkubwa ikizingatiwa kwamba walichapwa 2-0 nyumbani. “Kinachofanyika kwa sasa kinasikitisha sana, kwa wachezaji lakini toeni uamuzi kutuhusu mwisho wa msimu.

“Tumefikia mwisho wa mbio, ndefu sana katika Kombe la FA, kwa hivyo inasikitisha sana, na tunataka kuangazia mechi inayofuata.”

Aliongeza: “Tumeshindwa, ndio. Tunahuzunika lakini lazima tuangazie mechi inayofuata.

“Arsenal imeshindwa mechi nyingi kabla na tutashindwa siku zijazo. Lazima tusalie pamoja na kukabiliana na hali na kujiandaa kwa mechi ijayo kwa Imani.

“Mashabiki wanaunga mkono klabu na tunataka kupambana hadi mwisho wa msimu kila mechi.” aliongeza Wenger

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents