Burudani

Werrason agoma kushuka nchini

By  | WerrasonYule msanii ambaye aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na watanzania Ngiama ‘Werrason’ Makanda kutoka jamuhuri ya watu wa Congo, amegoma kushuka nchini kutokana na sababu sizizoeleweka na badala yake kupelekea mashabiki kurudishiwa tiketi ambazo walikuwa wameshazikata kwa ajili ya onesho hilo.

WerrasonYule msanii ambaye aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na watanzania Ngiama ‘Werrason’ Makanda kutoka jamuhuri ya watu wa Congo, amegoma kushuka nchini kutokana na sababu sizizoeleweka na badala yake kupelekea mashabiki kurudishiwa tiketi ambazo walikuwa wameshazikata kwa ajili ya onesho hilo.

 

Onesho hilo lilibatizwa jina la club E lilitarajiwa kufanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubelee chini ya udhamini wa TCC na sigara yao ya Embassy lakini ndo hivyo mchongo umefeli na kupelekea kutokufanyika kwa onesho hilo lililotarajiwa kuwa ni la kukata na shoka.

 

Makubabaliano yalikwishafanyika na mtu mzima Werrason alishathibitisha kufika nchini na taratibu zote zilikuwa zimekamilika lakini cha ajabu zilipofika nyakati za mchana jamaa alichomoa pasi na sababu yoyote, ili kutimiza azma yao, kampuni ya TCC ilibadili uamuzi kwa kufanya mazungumzo ya fasta fasta na mwanamuziki JB Mpiana Mukulu ili kuja kuliziba pengo hilo, na yeye alikuwa yuko tayari kuja lakini taratibu za safari zikawa ngumu kwani muda ulikwishapita sana na ndege zote kuwa zimejaa.

 

Aidha wadhamini hao walijaribu kufanya taratibu za kumtumia ndege nzima itakayombeba yeye na timu yake lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda hivyo kila kitu kikawa kimeharibika na mpaka tunaenda mitamboni hakuna kauli yoyote kutoka kwa watu wa TCC kuhusiana na hili.

 

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments