Michezo

Wigi lamponza mwanariadha wa Nigeria, Okagbare (Video)

Mwanariadha wa Nigeria, Blessing Okagbare amejikuta akifanya kituko asicho kitarajia katika mashindano ya mbio za wanawake za IAAF Diamond Oslo.

Mwanariadha wa Nigeria, Blessing Okagbare baada ya kuruka na kudondosha Wigi

Okagbare ambaye ni bingwa wa medali ya fedha katika mashindano ya Beijing mwaka 2008, ametoa kali ya mwaka katika mashindano hayo ya Oslo Diamond siku ya Alhamisi baada ya kujikuta Wigi alilovaa kichwani likianguka hadharani wakati akiruka.

Blessing Okagbare akiangaika kulirudisha Wigi kichwani

Baada ya kuvuka kwa wigi hilo mkimbiza upepo huyo wa Nigeria hakuonesha kushitushwa na kile kilichotokea na badala yake alikuwa makini na ugawaji wa alama zake ambazo ametumia.

Blessing Okagbare akiangaika kulirudisha Wigi kichwani

Habari njema kwake nikuwa alifanikiwa kufanya vizuri katika mashindano hayo baada ya kuruka umbali wa mita 6.21m.

Video inayo onyesha tukio la Blessing Okagbare 

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents