Burudani

Wiz Khalifa atengeneza rekodi mpya YouTube

Rapper Wiz Khalifa ajitengenezea rekodi mpya katika mtandao wa YouTube kwa kumbwaga Psy kutoka Korea Kusini.

Video ya wimbo wake ‘See You Again’ ambao aliuachia mwaka 2015 na kumshirikisha Charlie Puth imekuwa video ya kwanza ambayo imetazamwa zaidi katika mtandao huo amba mwanzoni msanii Psy kupitia video ya wimbo wake Gangnam ndio ilikuwa inaongoza.

Kwa sasa video ya Wiz imetazamwa mara 2,902,472,608 wakati ya Psy ikiwa imetazamwa mara 2,896,175,798. Wimbo huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya kifo cha Paul Walker aliyefariki mwaka 2013 kwa ajali ya gari.

Wiz Khalifa ameonekana kufurahishwa na mafanikio hayo na kuwashukuru mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika, “Thank you guys for making See you again the #1 most viewed video in YouTube history. Your love and support is very much appreciated. #tgod.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents