Yaya Toure atajwa tena kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika
Yaya Toure, ametajwa tena miongoni mwa wachezaji watatu bora kuwania taji la mwana soka bora mwaka huu na shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Tuzo hii huwajumuisha wachezaji wa Afrika wanaocheza soka ng’ambo.
Andre ‘Dede’ Ayew kutoka Ghana
Nyota huyo wa Manchester City kwa mara nyengine atakuwa akipigania taji hilo dhidi ya mshambulizi wa Black Stars ya Ghana na Swansea Andre ‘Dede’ Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund.
Pierre Emerick Aubameyang kutoka Gabon
Ikiwa atashinda kiungo huyo wa The Elephants ya Ivory Coast Yaya Toure, atakuwa mtu wa kwanza kunyakua taji hilo kwa mara ya tano.
Toure, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mapema mwaka huu pamoja na aliyekuwa nahodha wa Cameroon Samuel Eto’o ndio wachezaji wa pekee waliowahi kutwaa taji la mchezaji bora wa Afrika mara 4.
Eto’o alitwaa taji hilo katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.