Burudani

Young Killer kuachia albamu mbili mwaka huu

Msanii wa muziki Bongo, Young Killer amesema moja ya mipango yake kwa mwaka huu ni kutoa albamu mbili.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Toto Tundu’ ameiambia Clouds Fm kuwa ameshafanya ngoma nyingi na wasanii wa ndani na kutoka nje kitu ambacho anaamini hatua iliyobaki ni kutoa albamu.

“So kitu ambacho naweza kukifanya mwaka huu nitatoa albamu, I think zitakuwa ni mbili itakuwa na mix tap moja kwa hiyo wakae mkao wa kula mashabiki wangu,” amesema Young Killer.

“Mwaka huu sijapanga nitatoa ngoma ngapi, mwaka jana niliwahaidi nitatoa ngoma tano ndio zimetoka,” ameongeza.

Miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambayo wanatarajiwa kutoa albamu kwa mwaka huu ni Diamond Platnumz ambaye katika albamu yake itajayo ‘A Boy From Tandale’, Young Killer atakuwepo pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents