Habari

Zaidi ya wachimba madini 160 wafariki kwa kufunikwa na tope, Myanmar

Miili ya karibu wachimba migodi 160 wa madini ya jade wameopolewa kutoka kwenye tope baada ya maporomoko ya ardhi kutokea kaskazini ya Myanmar hii leo, katika mojawapo ya ajali mbaya kabisa kuwahi kuikumba sekta hiyo yenye hatari kubwa.

More than 100 dead in landslide at Myanmar jade mine

Mkasa huo umetokea baada ya mvua kubwa kunyesha karibu na mpaka wa China katika jimbo la Kachin. Idara ya Zima Moto ya Myanmar imesema wachimba migodi hao walifunikwa na wimbi la tope na mpaka sasa miili ya watu 162 imepatikana.

Polisi ya eneo hilo imesema waathiriwa walikaidi onyo la kutofanya kazi katika migodi hiyo wakati wa mvua. Shughuli ya utafutaji na uokozi imesitishwa kwa muda kwa sababu ya mvua kubwa.

Watu hufariki kila mwaka wakati wakifanya kazi katika sekta hiyo yenye faida kubwa, lakini isiyodhibitiwa ipasavyo ya madini ya jade, ambayo inawatumia wafanyakazi wahamiaji wanaopewa malipo duni kuchimba madini hayo yanayothaminiwa sana nchini China.

Shirika la habari la Deutsche Welle

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents