Soka saa 24!

Zidane: Nataka kuirejesha klabu hii pale ilipokuwa, nimepata nguvu mpya

Kocha mpya wa Real Madrid, Zinedine Zidane anaanza kazi leo, baada ya jana kutangazwa rasmi kuchukua mikoba ya Santiago Solari, aliyefukuzwa.

Zidane, anarejea Madrid, miezi 10 baada ya kuipa ubingwa wa Ulaya mara 3 mfululizo, akiwa na kibarua kigumu cha kurejesha makali ya timu hiyo, iliyoondolewa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya na Ajax kwa kipingo cha aibu cha 4-1.

Katika ligi kuu ya Hispania “Laliga” Madrid kwa sasa iko katika nafasi ya tatu, iizidiwa pointi 12 na vinara wa ligi hiyo, Barcelona.

Zidane amepewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wa Ulaya, na mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya wanahabari, Zidane,46, anasema ana furaha kurejea nyumbani.

“Nataka kuirejesha klabu hii pale ilipokuwa, ni ngumu sana kujua yanayoendelea ukiwa nje. Nimekuwa nikiishi Madrid, na kufanya mambo yangu hapa. Lakini sasa nimepata nguvu mpya, niko tayari kuiongoza klabu hii tena.”

Rais wa Madrid, Florentino Perez amemtaja Zidane kama mmoja wa makocha bora duniani.

“Kocha bora duniani amerejea kuungana nasi, malengo yetu ni kuwa wamoja tena.”

Kuondolewa huko Kwenye michuano ya Ulaya kunafuatia vipigo viwili kutoka kwa mahasimu wao, Barcelona. Walifungwa 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Laliga na kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-1 katika kombe la Copa del Rey.

Zidane alijiuzulu kuifundisha Madrid mwezi May mwaka jana kutwaa ligi ya mabingwa kwa kuifunga Liverpool, Julen Lopetegui alichukua nafasi yake kabla nay eye kutiuliwa muda mfupi kabla ya michuano ya kombe la dunia, kufuatia kukubalia kuifundisha timu ya taifa ya Hispania katika michuano hiyo.

Kocha wa timu ya akiba, Solari alipewa mikoba kabla ya kutimuliwa akiifundisha timu hiyo kwa miezi minne na nusu tu.

Zidane anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuijenga tena Madrid, ambayo tangu iondokewe na nyota wake, Chritiano Ronaldo, aliyejiunga na Juventus msimu huu, imeshindwa kufanya vizuri.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW