Burudani ya Michezo Live

Zimbabwe: Benk Kuu ya nchi hiyo yashindwa kutoa fedha mpya

Benki Kuu ya Zimbabwe imeshindwa kutoa noti mpya za kama ilivyotarajiwa, ambazo zitasaidia kupambana na upungufu wa fedha nchini humo pamoja na kukabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Uchumi wa Zimbabwe

Ilitangaza ingetoa noti za dola mbili na sarafu za dola tano, noti za kwanza za sarafu za kweli katika miaka 10.

Hata hivyo benki hiyo imejawa na hofu kwa sababu kitendo hiki kitachangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei, na kusisitiza fedha hizi hazitoongeza usambazaji wa pesa kwa ujumla.

Mwezi Juni mwaka huu benki kuu ilipiga marufuku matumizi ya dola za Kimarekani, zilizoanza kutumika mwaka 2009 kama njia mbadala ya fedha za ndani, kusaidia hali ya kiuchumi kurudi kawaida.

Serikali inasema fedha hizi mpya itapunguza upungufu wa fedha ambayo imesababisha watu wengi kutoweza kutoa hela zao zilizopo benki.

Hofu kubwa hapa ni uletwaji wa fedha hizi katikati ya matatizo ya kiuchumi itazidi kuchochea mfumuko wa bei.Fedha za zamani za ZimbabweFedha za zamani za Zimbabwe

Mkate uliokuwa unauzwa dola moja mwezi January, kwa sasa unauzwa kwa dola 15 za kizimbabwe. Tangu kurudishwa kwa fedha hizi, mfumuko wa bei umeongezeka mara tatu zaidi.

Serikali ya Zimbabwe imeacha kuchapisha takwimu rasmi, ila kwa sasa inasemakana kuwa inakiwango cha asilimia 300.

Benki kuu imeiambia BBC kuwa baadhi ya benki zimeanza kukusanya fedha mpya na zitaanza kusambazwa siku ya Jumanne.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW