298 hatiani kwa kuchochea mgomo wa daladala.

dldl_m.jpgPolisi wa mkoani Dar es Salaam wamewakamata watuhumiwa 298 katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Daladala Ubungo na Kituo cha Mabasi cha Mwenge, wakiwamo 111 wanaodaiwa kufanya uchochezi wa mgomo wa daladala nchini.

Polisi wa mkoani Dar es Salaam wamewakamata watuhumiwa 298 katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Daladala Ubungo na Kituo cha Mabasi cha Mwenge, wakiwamo 111 wanaodaiwa kufanya uchochezi wa mgomo wa daladala nchini.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jeshi hilo limewakamata watuhumiwa hao jana na watakaobainika kufanya uchochezi wa mgomo wa daladala, watachukuliwa hatua kali za kisheria. Kova alisema mgomo ambao ulikuwa ufanywe na madereva wa daladala haukuwa na ridhaa ya serikali,

Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Aliwataka wamiliki wa daladala na madereva wenye madai ya kupandisha nauli wafuate sheria na si kupandisha nauli kiholela, Pia aliwataka madereva wa daladala waendelee kutoa huduma za usafiri na si kugoma kabla sheria haijawafikia popote walipo.

Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki, Walukani Luhamba alisema nauli zitapanda baada ya kikao cha Bajeti kinachoanza leo kumalizika na si wakati huu kama ambavyo imeamuliwa kiholela.

Luhamba amewataka wamiliki wa daladala na madereva kusubiri mpaka Bajeti ya Serikali itakapopitishwa ndipo wakae pamoja na wadau wa sekta ya usafiri ili kupanga nauli mpya ambazo zitatangazwa na vyombo husika.

“Subirini Bajeti ipitishwe ndio tukae na kujadili nauli halali, lakini hivi sasa hatutavumilia daladala zitakazopandisha nauli, atakaepandisha nauli kwa sasa atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema ofisa huyo wa Sumatra.

Kova alisema Polisi katika msako huo wamekamata viongozi wa vikundi visivyo rasmi kwenye vituo hivyo vinavyojulikana kwa majina ya Mungiki, Ngumi Jiwe na Wakali Wadanta, kwani vikundi hivyo vimekuwa vikijihusisha na vitendo vya uporaji wa mizigo ya abiria, uvutaji wa bangi na kuleta kero kwa abiria.

Alisema vikundi hivyo havijasajiliwa kisheria na havikubaliki na madereva wa mabasi ya mikoani, madereva wa daladala na makondakta kwani wamekuwa wakiwatoza fedha madereva na makondakta hao bila ridhaa yao na endapo dereva, akikataa hutishiwa na kupigwa na vikundi hivyo jambo ambalo si haki.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents