Polisi wapora Milioni 4 na mbolea mifuko 640

Ikiwa inaendelea kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake, polisi wapatao watano wa kituo cha Chang’ombe wanadaiwa kumteka mfanyabiashara na kumpora fedha na mali.

Ikiwa inaendelea kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake, polisi wapatao watano wa kituo cha Chang’ombe wanadaiwa kumteka mfanyabiashara na kumpora fedha na mali.

Taarifa zilizopatikana katika kituo hicho jana, askari hao ambao mmoja ni koplo na wengine makonstebo, wanatuhumiwa kufanya ukatili huo juzi majira ya saa 12 jioni huko maeneo ya Temeke Vetenari.

Imedaiwa kuwa askari hao ambao majina yao tumeyahifadhi kwa sasa, walimkamata Bw. Fred Sanga, mkazi wa Kimara na kumpora sh. milioni nne na mbolea mifuko 640 yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 12.

“Baada ya kumkamata Vetenari walimlazimisha kuelekea Kigogo huku wakimfuatilia na gari lao na huko walimpora kila kitu na mzigo huo wa mbolea kuuza kwa mteja asiyefahamika mpaka sasa,”alisem msamaria mwema mmoja ambate hakutaka jina lake litajwe.

Hadi jana, habari zilisema askari wawili walikuwa tayari wamekamatwa na kuhojiwa, huku wawili wakiwa kwenye operesheni maalumu, lakini tayari wamepewa mwito wa kufika kituoni kwa mahojiano.

Habari zilisema askari mmoja hadi jana alikuwa hajaonekana kituoni hapo, huku akidai kuwa anaumwa na amelazwa Kinondoni na watatu kati yao ni madereva wa Polisi.

Mpaka sasa polisi hao wamefunguliwa kesi namba CHA/RB/5045/08 na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Temeke, Bw. Hamisi Olotu.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents