Burudani
Mrisho Mpoto aeleza ni Wizara gani ya serikali anaweza kuimudu kama akipewa nafasi
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amesema kama angepata nafasi ya kuteuliwa na kuwa katika Wizara ya Habari, Utamudini na Michezo basi angehakikisha ulimwengu unaujua utamaduni wa Tanzania.
Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Mpoto alidai Tanzania bado haijanufaika vizuri na utamaduni wake.
“Mimi ningependa Wizara ya Habari, Utamudini na Michezo kwa sababu nataka kuuambia ulimwengu kwamba tuna makabila 120, tuna lugha 132, tuna vyakula, tuna mavazi, tuna kila kitu, huu wote ni mtaji tosha lakini havijulikani katika nyanja za kimataifa, tumevikalia sisi wenyewe ,” alisema Mpoto.
“Kwahiyo mimi ningelichukua swala zima la utamaduni kwa sababu Tanzania tunavitu vingi sana vinapotea,” aliongeza.