Nyota wa Bollywood Sanjay Dutt atoka jela
Nyota wa filamu za Bollywood, Sanjay Dutt ameachiwa kutoka jela alipokuwa amefungwa katika mji wa magharibi wa Pune nchini India.
Dutt mwenye umri wa 56 alihukumiwa kifungo jela kufuatia makosa ya kumiliki silaha inayohusishwa na mlipuko wa 1993 mjini Mumbai ambapo takriban watu 257 waliuawa na wengine 713 kujeruhiwa.
Dutt alipatikana na hatia ya kununua silaha hiyo kutoka kwa walipuaji ,lakini yeye akasema kwamba silaha hiyo ilikuwa muhimu kwa lengo la kuilinda familia yake wakati wa ghasia za Waislamu dhidi ya Hindu.
Baadaye alipelekwa hadi jela ya Pune mwaka 2013 ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano. Hata hivyo alipewa msahama wa siku 144 baada ya kuonekana kuwa na tabia njema na vitendo kama vile kusimamia kipindi cha redio.
Source: BBC