Michezo
Leicester wanaukaribia ubingwa wa EPL baada ya kuifunga Newcastle
Klabu ya Leicester City wamezidi kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi dhidi ya Newcastle.
Lecester waliiifunga Newcastle, waliokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza chini ya meneja mpya Rafael Benitez, kwa bao 1-0 mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu usiku.
Shinji Okazaki ndiye aliyewafungia bao hilo la pekee, na alilifunga kwa ustadi wa aina yake dakika ya 25.
Leicester City sasa wanazidi kukaribia kushinda taji lao la kwanza kabisa la ligi zikiwa zimesalia mechi nane msimu huu.
Newcastle walionekana kuimarika na walikaribia kufunga kupitia Ayoze Perez na Moussa Sissoko lakini bahati yao haikuwa yao.