Burudani

Chill Na Sky: Haya ni Mambo 11 huenda ulikuwa hujui huhusu Shaa (Audio)

Haya ni Mambo 11 huenda ulikuwa hujui huhusu Shaa.

20160314214757

1. Alizaliwa mwaka 1985

2. Ni mtoto wa mwisho, kwenye familia ya watoto wanne

3. Baba yake ni mzaliwa wa Kyela, mama yake ni mzaliwa wa Nachingwea

4. Anatoka kwenye familia ya muziki, kaka yake ni msanii wa reggae, anaitwa Ras Gwandumi, dada yake Nelu Kaisi ni mpiga gitaa la base

5. Baba yake, Dr Kaisi (amestaafu mwaka 2015) ni bingwa wa magonjwa wa wanawake Tanzania. Alikuwa akiwatibu wake wa marais wa Tanzania

6. Mama yake alikuwa Kabidhi Wasii Mkuu wa serikali wa kwanza mwanamke

7. Akiwa amemaliza kidato cha nne, hakuwa amepanga kushiriki kwenye Coca Cola Popstars, alimsindikiza rafiki yake (Zubeda) ambaye hakutokea. Wakati anasubiri wahusika walimuambia aimbie tu lakini akaonesha maajabu na akachaguliwa. Top 6 waliingia yeye, Langa, Witness, Terrence, Illu na Enika

8. Alipata scholarship na kwenda kusoma sanaa (Arts and Design) Washington DC, Marekani. Ni mchoraji mzuri wa picha. “Nachora kila kitu.”

9. Jina lake Shaa alipewa na marehemu Ngwair. Lilitoka kwenye jina Wakilisha (SHA) aliongeza A mwishoni na kuwa SHAA

10. Alikuwa msanii wa kwanza wa kike kusainishwa na label ya MJ Records

11. Mwanzoni Master J alikuwa akimchana na kuhisi kuwa hakustahili kushinda mashindano ya Popstar. Anasema hiyo ilimjenga na kumtengeneza kuwa msaniii mzuri

Sikiliza kipindi chote hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents