Michezo
Man City Yaichakaza Liverpool
Man City imefanya mauaji makubwa baada ya kuifunga liverpool tatu bila katika ligi kuu ya England
Man City ilipata bao dakika ya 13 baada Gareth Barry kufunga bao la kwanza, kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Yaya Toure,Adan Johnson na James Milner .
Carlos Tevez alifunga bao la pili dakika 55 kutokana na mabeki wa Liverpool kushindwa kuokoa kona . Tevez alionyesha ustadi wake baada ya kufunga kwa penalti dakika 67 baada ya Adam Johnson kumuangusha Martin skrtel ndani ya eneo la hatari .
Man City ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na ushindi huo ulistahili kwani hawakuwa tishio kama wapinzani wao.
Kocha wa Man United Alex Furguson alikuwepo jukwaani akiangalia kwa makini mpambano huo.