Burudani
Azealia Banks asaini mkataba na RZA Records
Rapper wa kike kutoka Marekani, Azealia Banks amesaini mkataba na kampuni mpya ya RZA Records.
Kabla ya kusaini mkataba na lebo ya Epic Records, Banks aliwahi kuwa chini ya lebo kadhaa zikiwemo XL Records, Interscope Records, Polydor Records na Prospect Park Records.
“I’m FINALLY getting a record deal :),” ameandika kwenye mtandao wake wa Facebook. “I’m signing with RZA. He and I have an excellent work chemistry. Filming Coco with him was loads of fun!! Now I get to make music with him!!! Business and Pleasure is imminent.”
Hivi karibuni Azealia anatarajia kuachia albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Business and Pleasure’ japo haijajulikana siku maalum ya kutoka.