Michezo

Matokeo ya ligi kuu Tanzania Bara Simba na Yanga zapata ushindi Azam ya chapwa

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) iliendelea October 12 2016 katika viwanja mbalimbali, klabu ya Simba ikicheza mchezo wake wa kwanza ugenini katika dimba la Sokoine waliibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Simba walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Ibrahim Ajibu ‘Fundi’, ambaye alipiga mpira wa adhabu na kutinga moja kwa moja wavuni, Shiza Kichuya alifunga bao la pili mnamo dakika ya 33 na kuandika bao lake la sita msimu huu akiwa ndio kinara wa mabao.

Yanga nao wakachomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wakatamiwa na Mtibwa Sugar. Mwadui Fc wakawachapa African Lyon kwa mabao 2-0. Chama la wana Stand United wamewachapa wanalamba lamba Azam FC kwa bao 1-0.

Jkt Ruvu na Tanzania Prisons wametosha nguvu kwa sare ya bila kufungana. Nao Mbao Fc waliwachapa ndugu zao Toto Africans kwa mabao 3-1.
Majimaji wamelala nyumbani kwa kuchapwa kwa bao 1-0 na kagera Sugar.

Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa Kwa Ruvu Shooting kuwa wenyeji wa Ndanda.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents