Zimesalia siku chache Philippe Coutinho kujiunga na Barcelona – Segura
Meneja Mkuu wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Josep Segura amesema wanakaribia kuinasa saini ya mbrazili, Philippe Coutinho anayekipiga Liverpool na Ousmane Dembele wa Borussia Dortmund.
Mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho
Coutinho amekuwa akihusishwa kujiunga na vijana wa Camp Nou baada ya timu hiyo kutuma maombi ya kumsajili ndani ya Anfield na sasa anaaminika kuwa zinaisabiwa siku tu licha ya Liverpool kusisitiza kuwa kamwe haitamuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili na kukataa dau la pauni milioni 90.4 kutoka Barcelona.
Wakati mchezaji wa klabu ya Dortmund na timu ya taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele nimiongoni mwa wachezaji ambao wanatarajia kuwasajili wakiwa wametoka katika machungu ya kukubali kipigo cha jumla ya magoli 5-1 kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid katika mchezo wa Super Cup ya Hispania.
Wakati mchezaji wa klabu ya Dortmund na timu ya taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele
Segura amesisitiza kuwa Barca itakamilisha usajili wake baada ya kuwasajili wachezaji hao wawili ili kuziba nafasi iliyo achwa na Neymar ambaye amejiunga na matajiri wa Ufaransa Paris Saint-Germain kwa rekodi ya dunia ya dau la pauni milioni 222 mapema mwanzoni mwa mwezi huu.
By Hamza Fumo