Burudani

Alikiba aanza kutema cheche za Kipusa ‘they call me a heartbreaker?’

Msanii wa muziki, Alikiba kutoka RockStar4000 ametangaza ujio wake mpya baada ya ukimya wa muda mrefu.


Alikiba

Hit maker huyo wa ‘Aje’ amekuwa na utaratibu wa kutoa ngoma chache kwa mwaka hali ambayo inawafanya mashabiki wake kuwa na shauku kubwa ya kusikia kazi zake mpya.

Wiki hii muimbaji huyo ameanza kuibua matumani mpya kwa mashabiki wake baada ya kuanza kutoa dondoo kuhusu ujio wake mpya ambapo alipost picha katika mtandao wake wa Instagram na kuandika wananiita ‘Kipusa’.

Katika picha nyingine muimbaji huyo amepost picha na kuandika “they call me a heartbreaker?#kingkiba” kauli ambayo imewafanya mashabiki wengi wa muimbaji huyo kuwa na shauku kubwa na kazi mpya ya muimbaji huyo baada ya Diamond anayedaiwa kuwa mpinzani wake kuachia nyimbo nyingi mfululizo.

Mpaka sasa Diamond tayari ameachia wimbo, Eneka, I Miss You, Fire akiwa akiwa amemshirikisha Tiwa Savage pamoja na Marry You aliyomshirikisha muimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo.

Mpaka sasa Alikiba bado hajaweka wazi ni lini ataachia kazi yake hiyo mpya inayosubiriwa kwa hamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents