Mjukuu akuta Lamborghini na Ferrari kwenye gereji ya bibi yake baada kupita zaidi ya miongo miwili
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Eriegin amesema kuwa katika hali isiyo ya kawaida amefanikiwa kuyaona magari mawili ya kifahari ya Lamborghini Countach na Ferrari 308 kwenye gereji ya bibi yake baada ya kupita zaidi ya miongo miwili toka kufariki kwake.
Mjuku huyo ambaye ni mwanafunzi ameyasema hayo huku akiposti picha za magari hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Reddit nchini Marekani na kuzua gumzo kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Kijana huyo alivunja na kuingia ndani ya gereji hiyo ambayo iliachwa kutumika kwa kipindi kirefu na kukuta magari hayo Lamborghini Countach aina ya silva na Ferrari 308 nyekundu yenye thamani ya pauni 430,000.
“Babu yangu aliyanunua magari haya mwaka 1989 kwaajili ya kumsaidia katika biashara zake lakini kutokana na kupandishiwa bima kwa muda huo alishindwa kuendelea kuendeleza kampuni yake na hivyo kupelekea kuhifadhiwa kwenye gereji kwa kipindi chote hicho cha zaidi ya miaka 20,”amesema kijana huyo aliyetumia jina la Eriegin.
Mamia ya watu kwenye mtandao huo wa kijamii walikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu wengine wakiuliza kwa nini yalikuwa hapo muda wote na hata wengine kufika mbali zaidi kwa kuhitaji kuuziwa magari hayo kutoka kwa kijana hiyo.
Wakati kijana huyo akisema kuwa amefurahi mno kupata magari hayo licha ya kumkumbusha machungu ya wazee wake na kuongeza amejiskia vibaya kutokana na kuwa magari hayo yalikuwa yamefichwa kwa kipindi chote hicho na kuahidi yatakuja kusaidia familia mara baada ya kukamilika marekebisho yake.
Imaitwa zalinusilonlitajarajia
Duniani mambo kama yote
Duh apo umaskini kwaheri
Hiyo model ya kfungua mlango kwa juu,ukisema zaidi ya miongo miwili manake ni miaka zaidi ya ishirini wakati kuanzia 97 kurud nyuma hiyo teknolojia ilikua bado.
Mapicha picha tu wanatuletea
sisi wengine tumeachiwa vyungu vya kupikia mlenda dah
Uwongo uwongo tu.
No research no right to speak
Sio kweli, Lamborghini yakwanza was built in 1963
Umemfumbua macho huyo alosema tecnolojia ilkua bado
Ally Blender tatizo nikuwahi ku comment bila kufikiria wala kuwa na ushahidi
Emmanuel Bandimakate alafu alivyo jeuri hadi saivi ajafuta comment yake… Ningekuwa mimi ningeshafuta kitambo..Kujifanya Unajua kumbe Hujui ni Ujinga 😅😅
ttz wtz wenzang ni wavivu kusoma😂
Fedo Mathube Jr., tatizo ni kwamba, yeye akiona gari ya staili fulani imeingia nchini kwetu na yeye anajua kua ndio ya mwaka huo, kumbe ina miaka kama kumi naa… Kwa mfano sa hiv unaeza nunua gari ilotoka 2002 lkn kwa huku ndio iko sokoni
Fedo Mathube Jr. Nakubaliana nawewe 100%
Mudathir El-salmy umeniuwa nacheko
Ha ha ha unatoka kijiji gani kwani
Uarabuni yani 💥💥💥🔫