Habari

FAHAMU: Faini utakazotozwa endapo utagonga aina hii ya wanyamapori mbugani, Chui faini yake kubwa kuliko Pundamilia

Kama ulikuwa unajiuliza ni faini ya shilingi ngapi utachajiwa, endapo ikatokea bahati mbaya ukagonga mnyama kwenye barabara zinazokatiza kwenye hifadhi, kama ile ya Dar Es Salaam – Mbeya ambayo inakatiza katika Mbuga ya Taifa ya Mikumi, basi hapa chini tumepata baadhi ya faini utakazochajiwa endapo ikitokea ajali hiyo.

Kabla ya kufikiria faini, kwanza ni vyema ukafuata sheria na kanuni zilizowekwa pindi unapokatiza kwenye Mbuga au Hifadhi husika ili kuzuia ajali za kizembe.

Hizi ni baadhi ya tahadhari zilizowekwa kwa ajili ya usalama wako binafsi na usalama wa wanyamapori. Sasa haya ni mambo ambayo hutakiwi kufanya kabisa.

1. Hutakiwi kulisha wanyama au kutupa kitu kama chupa au kopo mbugani, maana unaweza leta shida kwa mnyama ataekula .


2. Hutakiwi kusababisha ajali ya aina yoyote Mbugani. Kwa kawaida spidi ya mchana mbugani ni 70km/h na usiku ni 50km/h.


Hizi ni baadhi ya faini ambazo utatozwa endapo utagonga mnyamapori mbugani na hii ni kwa hapa kwetu Tanzania.

TEMBO = USD 15,000 ~ Tsh mil 35.1
NYATI = USD 1,900~ Tsh mil 4.3
SIMBA = USD 4,900~ Tsh mil 11.3
CHUI = USD 3,500~ Tsh mil 8
TWIGA = USD 15,000~ Tsh mil 34.6
FISI = USD 550~ Tsh mil 1.2
NGIRI = USD 450~ Tsh mil 1
NYANI = USD 110~ Tsh laki 254
PUNDAMILIA = USD 1200~ Tsh mil 2.7
SWALA = USD 390~ Tsh laki 9

Na endapo ukipata ajali ndani ya Mbuga faini yake hutozwa Tsh 200,000 na ukizisha mwendo kwenye hifadhi faini yake ni Tsh . 30,000/= .

Unaweza ukasoma zaidi hapa:  https://www.instagram.com/p/BvJaE0hDByi/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents