Picha
Picha: Wema Sepetu aionesha gari yake mpya
Unamkumbuka Vannie? Mtoto wa Wema Sepetu (mbwa). Hivi karibuni (kwa lugha ya picha) amepata ndugu yake japo si mbwa kama yeye, ni gari. Picha za Gari hiyo aina ya Audi Q7 yenye rangi nyeusi inaonekana kwenye akaunti ya Wema ya Instagram alipokuwa beach hivi karibuni na kuiandikia caption, ‘my baby at da beach.’
Kwenye akaunti ya meneja wake Martin Kadinda pia kuna picha nyingine ya gari hiyo aliyoiandikia maneno, ‘#maisha sio manhattan…..You can creat your own Manhattan in Tz… Hata kama ni Ya muda mfupi… #Kiphating.’
Gharama ya gari hiyo inaweza kuanzia shilingi milioni 70 na kuendelea.