Habari
Mr Nice kusaini mkataba na kampuni mpya Alhamis hii jijini Nairobi
Kwa mara nyingine tena, Mr Nice anatarajia kusaini mkataba mnono mbele ya waandishi wa habari jijini Nairobi, Kenya.
Nice atasaini mkataba mpya na ‘Candy n Candy Records’ Alhamis hii, July 25 kwenye kiota cha Lavish Lounge mida ya saa tano asubuhi.
Siku hiyo, Mr Nice ataongelea pia shutuma za ulevi, uzembe na uzinzi dhidi yake zilizodaiwa kuwa ni sababu za kupigwa chini na Grandpa Records.
Mr Nice alifukuzwa Grandpa Records huku baadhi ya mashabiki wakimcheka kuwa alienda Kenya kwa ndege lakini akaondoka kwa basi.
Source: Ghafla Kenya