Burudani
Rihanna: Sipendi kujirusha tena
Huenda kwa kumuangalia Miley Cyrus akitikisha makalio yake aka twerk kunatosha kuumaliza kabisa mzuka wa Rihanna kukesha kwenye club za usiku siku hizi.
Muimbaji huyo wa Diamonds amesema maisha yake yamebadilika. “Siku hizi sipendi kujirusha,” alisema Rihanna kwenye kipindi cha TV cha Chatty Man. “Sijui kama ni visigino vyangu… sipendi kusimama muda mrefu. Sijui kama ni hivyo, lakini nimekuwa nikiboreka sana.”
“Sijui ni kwasababu ni muziki ule ule kila siku. Pengine tunahitaji madj wengine.”