MMC: Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz waitawala Marimba Music Chart wiki hii (11th October 2013)
Wiki hii mastaa wa muziki wa kizazi kipya ambao pia ni maswahiba Omary Nyembo aka Ommy Dimpoz na Abdul Naseeb aka Diamond Platnumz ndio wanaoitawala chart ya muziki ya Marimba kwa kushika nafasi muhimu za juu kabisa.
Ikiwa ni wiki ya 11 ya MMC, ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz imeendelea kukamata nafasi ya 1 kwa wiki ya pili, wakati ‘My Number One’ ya Diamond imekwea mpaka nafasi ya pili tokea nafasi ya nne wiki iliyopita.
Hii ni chart rasmi ya muziki wa kizazi kipya Tanzania ‘Marimba Music Chart’, inayotokana na chart za radio mbalimbali za Tanzania. Yapo mabadiliko machache katika chart ya wiki hii.
Marimba Music Chart (MMC) huandaliwa na BONGO 5 kila wiki kutokana na Chart za Radio mbalimbali (zinazowakilisha radio zote) Tanzania.
HII NDIO CHART RASMI YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA WIKI HII (11th October 2013)
Ingia HAPA kupata chart ya Marimba ya wiki iliyopita (03rd Oct 2013)
VYANZO:
VIGEZO:
MMC inatumia Chart za radio mbalimbali za Tanzania (sample) kuchuja na kupata orodha ya nyimbo zilizoingia katika chart nyingi zaidi na kupata nyimbo 20 ambazo ndio zinazofikia kigezo cha kuingia katika Marimba Music Chart.