Michezo
TP Mazembe ya Ifunga 1-0 Zamalek na Kuongoza Kundi A
Club ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliishinda Zamalek ya Misri kwa goli 1-0 kwenye mechi za makundi ya Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika siku ya June 8 Jumapili
Mchezaji kutoka Zambia Rainford Kallaba alifunga goli pekee lililoipa ushindi TP Mazembe. Kwa matokeo hayo ya Lubumbashi yanamaanisha kwamba Mazembe wanaongoza kundi A kwa alama sita.
Wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club wako nafasi ya pili, wakipitwa kwa alama mbili.
AS Vita walitoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Sudan Al Hilal siku ya Ijumaa.
Kwa upande wa kundi B, Entente Setif ya Algeria walibanwa mbavu kwa sare 1-1 nyumbani kwao na Al Ahli Benghazi ya nchini Libya.