BurudaniHabariLifestyleMitindo

Abuni vazi lenye thamani ya $8,900 Tsh Milioni 20

Mwanamitindo maarufu nchini Nigeria na Mbunifu wa mavazi Yomi Casual ameonyesha Shati lake alilosema lina thamni ya $8,900 sawa Tsh 20,754,800/= yaani milioni 20 shati hilo linaelewa kuwa limetengenezwa na yeye kama Mbunifu wa Mitindo ya mavazi kutoka nchini humo Nigeria.

Mbunifu huyo mashuhuria kutoka Nigeria hivi majuzi kupitia ukurasa wake wa Instagram alizindua muundo mpya wa kuvutia unaojumuisha shati nyeupe ya vifungo huku ndani ikionekana T-shirt nyeusi lakini shati likiwa limechomwa kwamoto.

Katika nukuu yake, alifichua kuwa kipande hicho kiligharimu karibu Naira 3,898,200 sawa dola za Kimarekani ($8,9000) lakini kwa fedha za Kitanzania ikiwa ni Tsh milioni 20 na akawataka mashabiki kuwatambulisha watu mashuhuri ambao walidhani wangevaa muundo huo.

Ameandika kuwa: “Exclusively made for HIM. Please tag that celebrity that will k!ll this look…..👇🏿

PRICE : $8900″

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents