Habari

ACT-Wazalendo watoa sababu ya Mh. Zitto kukutana na viongozi wa upinzani

Baada ya kuenea kwa picha za Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya upinzani hatimae chama hicho kimeeleza kuwa kiliazimia kuanza kufanya mazungumzo na viongozi wengine wa vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia.

Akiongea na Bongo5 leo, Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Ndugu.Ado Shaibu amesema kuwa ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake.

“Kamati Kuu ya Chama chetu iliazimia kuwa Uongozi wa juu wa Chama uanze mazungumzo na viongozi wengine wa Vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia. Ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake. Moja ya mambo hayo ni mapambano ya kidemokrasia kwa hiyo, Zitto amekwishafanya mazungumzo na Mbowe na Rungwe na atafanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vingine,” amesema Ado.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents