ACT yasisitiza kufutiwa kesi

Chama cha ACT Wazalendo kimehimiza, kufutwa kwa kesi za uchaguzi zinazowakabili wao pamoja na vyama vingine vya upinzani zilizotokana na uchaguzi Mkuu wa 2020.

Katibu Mkuu ACT, Ado Shaibu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndg, Ado Shaibu ambapo ameeleza kuwa msimamo huo ni sehemu ya mambo ambayo Kiongozi wa Chama chao, Zitto Kabwe aliyaanisha kwenye barua ya kumuomba Rais Samia Suluhu, kuchukua hatua ili chaguzi nchini ziwe za huru, haki na kuaminika.

Shaibu amefafanua kwamba licha ya Tume za kusimamia Uchaguzi NEC na ZEC kuboresha baadhi ya maeneo bado yapo maeneo machache yanayohitaji kuboreshwa ikiwa ni pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama kutenda haki kwenye chaguzi zote.

Aidha Katibu Mkuu huyo amefafanua kwamba, barua ya Zitto kwenda kwa Rais Samia imeanisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzishwa majadiliano ya vyama ili kujenga kuaminiana, kutatua migogoro kwa njia ya amani, na michakato ya Katiba Mpya ili kujenga mazingira mazuri ya kisiasa, uchumi na kijami.

Hata hivyo, Shaibu ameweka wazi kwamba, barua ya kiongozi wao ilijibiwa na Rais Samia na kwamba Serikali ya awamu ya Sita ina dhamira ya kuimarisha demokrasia nchini.

BY : Fatuma Muna

 

Related Articles

Back to top button