Burudani

Afande Sele ampongeza RC Makonda kwa hili…

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Afande Sele ambaye zamani alikuwa mwanachama wa ACT Wazalendo kabla ya kukikacha chama hicho, Jumatatu hii ameibuka kwa kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kitendo chake cha kuyakusanya magari mabovu ya askari ya kwenda kuyakarabati.

RC Makonda akiwa kwenye magari hayo pamoja na polisi

Rapa huyo amesema kitendo cha mkuu huyo kimeonyesha taswira tofauti huku akidai zamani magari ambayo yalikuwa yanachakaa yalikuwa wanauzwa kwa watumishi wa jeshi hilo kwa bei ya chini.

“Ingekuwa zile siku za zamani kidogo haya magari aliyoyakarabati huyu mkaka wa Dar wangeuziana mabosi wa polisi na wapendwa wao kwa shilingi laki mbili kila moja kama vyuma chakavu,” aliandika Afande Sele.

Aliongeza, “Katika hili huyu jamaa wa Dar anastahili kongole lakini yale mengine mimi hayanihusu bora nikae kimya kwanza kwetu sio Dar,”

RC Makonda hivi karibuni alikabidhi magari ya kisasa 18 kwa  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Magari hayo ni kati yale 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu kwaajili ya kufufuliwa upya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents