Burudani

Afande Sele asema hana mpango wa kuoa lakini

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop kutokea Morogoro, Afande Sele amefunguka kwa kusema kuwa hana mpango wa kuoa leo wala kesho.
Afande Sele akiwa na watoto wake Mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa
Afande Sele akiwa na watoto wake Mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa

Rapper huyo ambaye ni baba wa watoto wawili, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha Eat Africa Radio kuwa kwa sasa ana jukumu kubwa la kuwalea watoto wake ambao mama yao alishafariki dunia.

“Niwe mkweli tu hilo wazo la kuvuta jiko sina, namshukuru Mungu nimepata watoto wawili naweza kwenda nao vizuri na kuwalea, kusema nifunge ndoa leo au kesho utakuwa uongo sababu ndoa si kusema mwanamke kuchukua nyanya tu gengeni,lazima nipate mwanamke amabaye atakuwa na vigezo vya kuwa na mimi atajua nini maisha ambayo mimi nayahitaji, atanielewa tabia zangu za nje na ndani hivyo sidhani kama ni rahisi kupata mke kwa kipindi hiki ila najivunia kuwa na marafiki ambao wanasaidia kulea watoto wangu, wanawapenda watoto zangu hicho nashukuru” alisema Afande Sele.

Aliongeza, “Nipo kwenye kupima nawapima na wao wananipima mimi, mimi na marafiki wa hivyo wakati ukifika nikiona yupo anafaa kuwa na mimi nitakuwa naye lakini niwe mkweli, siko mwenyewe au kusema natumia sabuni hapana mimi na warembo kama kawaida, wananisaidia kukaa na watoto wangu, wanaheshima. Maana mimi ni kama mfalme hata mfalme Suleman alikuwa wa wake zaidi ya mia tatu kwenye nyumba yake, hata mimi wapo kadhaa ila hawazidi sita” aliongeza Afande Sele

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents