Michezo

Afisa wa idara ya uhamiaji Dar awataja wachezaji wa Simba na Yanga wasiokuwa na vibali

Baada ya siku moja idara ya uhamiaji kuviambia vilabu vya soka vya Simba na Yanga kutowachezesha wachezaji wake wasiokamilisha taratibu za kuishi na kufanya kazi nchini, afisa wa idara ya uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam, John Musumule amefunguka.

Afisa Musumule amekiambia kipindi cha Sports HQ cha EFM kuwa kuna baadhi ya wachezaji na makocha wa timu hizo hawana vibali vya makazi na vile vya kufanyia kazi hapa nchini.

Akiongelea kwa upande wa Simba, Musumule amedai baadhi ya wachezaji wa timu hiyo hawana vibali vya makazi na wengine hawana vibali vya kufanyia kazi na wengine hawana vyote kwa pamoja wakiwemo na makocha wao wakigeni.

Kwa upande wa Yanga amesema kuwa makocha wa timu hiyo amebahatika kuwa na vibali vya makazi hapa nchini lakini hawana vibali vya kufanya kazi. Wakati huo huo ameipongeza timu ya Azam FC kuwa haina tatizo lolote imekamilisha na kufuata taratibu zote kwa wachezaji wake.

Afisa huyo ameongeza kuwa kwa wachezaji wote wasiokuwa na vibali hivyo hawatakiwi kushiriki kwenye mchezo wowote na endapo timu itakiuka maagizo hayo watachukua hatua kali za kisheria ikiwemo kumfikisha mchezaji na timu yake mahakamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents