Habari

Ajali ya Treni na Basi yaua watu 10 Kigoma, Zitto Kabwe achukua maamuzi haya

Watu 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine 26 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wanasafiria kugonga Treni la mizigo.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imehusisha Basi la kampuni ya HAMIDA lililokuwa likisafiri kutoka Kigoma kwenda Nzega, Tabora kugonga treni ya mizigo leo Juni 6 majira ya asubuhi katika eneo la Gungu, Kigoma.

Hata hivyo, Kamanda Martin Otieno amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa kukatiza reli bila kuzingatia kanuni.

Kufuatia ajali hiyo, Mbunge wa kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa tayari ameshachukua uamuzi wa kuweka matuta katika eneo hilo ambalo amelitaja kuwa ni eneo hatari kwani huwa panatokea ajali mara kwa mara.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema kuwa tayari ameshawasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania na wamekubaliana kuweka kizuizi ( matuta ) Katika eneo hilo ili kupunguza ajali.

Chanzo:ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents