HabariSiasa

Ajali yaua 35 wakielekea Kanisani kwaajili ya Pasaka Zimbabwe

Watu wasiopungua 35 wamefariki na wengine 71 wamejeruhiwa baada ya basi lililokuwa limewabeba watu waliokuwa wakielekea kanisani kwa ajili ya Pasaka kuacha njia na kuanguka kwenye korongo katika mji wa kusini mashariki mwa Zimbabwe wa Chipinge.

Polisi wametoa taarifa leo ambapo msemaji wa polisi ambaye ni naibu kamishna, Paul Nyathi, ameliambia shirika la habari la AFP, ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo na hadi sasa watu waliokufa ni 35.

Gari lililopata ajali lilikuwa likiwasafirisha waumini wa kikristo wa kanisa linalojiita la Kizayuni ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wa Pasaka kusini mwa nchi hiyo.

Imeelezwa kwamba ishara zimeonesha basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kinachotakiwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents