Habari

Aliyekuwa Rais wa Chad Idriss Deby kuzikwa leo

Chad leo inafanya mazishi ya kiongozi wake wa muda mrefu Idriss Deby aliyefariki dunia mapema wiki hii wakati wasiwasi unaongezeka juu ya hatma ya demokrasia kwenye taifa hilo la kanda Sahel.

Viongozi kadhaa wa ulimwengu akiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye taifa lake ni mkoloni wa zamani wa Chad wanahudhuria hafla ya mazishi ya kitaifa inayofanyika kwa heshima zote za kijeshi mjini N’Djamena.

Hafla hiyo itafuatiwa na ibada ya kidini kwenye msikiti mkuu mjini N’Djamena na baadae mwili wa Deby utasafirishwa na kuzikwa kwenye kijiji alikozaliwa mashariki ya nchi hiyo karibu na mpaka na Sudan.

Kifo cha Deby, aliyeiongoza Chad kwa zaidi ya miongo mitatu kilitangazwa na jeshi la nchi hiyo siku ya Jumatatu kutokana na kile kilichotajwa kuwa majereha aliyoyapata akiwa mstari wa mbele kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya waasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents