Amuua Mtoto kwa kumnywesha sumu ya panya

Mwanamke mmoja mkazi wa Mwakibete mkoani Mbeya aliyejulikana kwa jina la Bibi Sikujua John (31) anashikiliwa na Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuua mwanawe kwa kumnywesha sumu ya panya

Mwanamke mmoja mkazi wa Mwakibete mkoani Mbeya aliyejulikana kwa jina la Bibi Sikujua John (31) anashikiliwa na Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuua mwanawe kwa kumnywesha sumu ya panya.

 

 

 

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bw. Suleimani Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa awali, mwanamke huyo alimpeleka mtoto huyo Veronica Geofrey mwenye umri wa miezi minne hospitali na kumweleza daktari kuwa alikuwa na hali mbaya na kutapika sana lakini baada ya uchunguza, daktari aligundua mtoto huo alikuwa akitoa harufu ya sumu ya panya mdomoni na kumweleza mama huyo kwamba amempa mwanawe sumu ya panya jambo ambalo Mama huyo alikiri kulifanya.

 

 

 

Baada ya muda mfupi kupita mtoto huyo alifariki dunia ndipo daktari huyo alipotoa taarifa kituo cha polisi, bila kuchelewa askari walifika na kumtia nguvuni mama huyo na Alipohojiwa alikiri kumnywesha sumu mtoto huyo.

 

 

 

Alidai sababu zilizopelekea yeye kufanya hivyo, eti kwa kuwa ana watoto wengine wawili ambapo mmoja ni marehemu ambao wamefuatana sana hivyo aliamua kuua mtoto huyo kutokana na kunyanyaswa na mumewe ambaye hampi matunzo hivyo alidhania kuwa hiyo itakuwa ni njia rahisi ya kupunguza makali ya ugumu wa maisha.

 

 

 

Juhudi za kutafuta Mume wa Mwanamama hyo zilizaa matunda na alipohojiwa kuhusu madai ya mkewe, Jamaa alikana kutompa pesa za matumizi mkewe.
Mpaka sasa mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.

 
Wakati huko nako Kagera Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia, Bi. Adventina Samson (44) mkazi wa Kagemu Kitendaguro kwa tuhuma ya kumuua mumewe kwa kumchoma kisu kifuani katika ugomvi wa kifamilia.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents