Wanazuoni watumie Lugha ya Kiswahili – Mkuchika

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amewaonya wanazuoni mahiri wa lugha ya Kiswahili na maprofesa kwamba, iwapo lugha za Kiafrika hazitaandikwa zitakuwa katika hatari ya kufa

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amewaonya wanazuoni mahiri wa lugha ya Kiswahili na maprofesa kwamba, iwapo lugha za Kiafrika hazitaandikwa zitakuwa katika hatari ya kufa hivyo ni vema kuzikomalia lugha zetu.

 
Akifungua kongamano la maprofesa kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuhusu lugha katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ACALAN), Mkuchika alisikitishwa kuona nchi za Ulaya zinavyozidi kuzienzi lugha zao lakini Afrika hali ni tofauti watu wanaona aibu kutumia lugha zao na kujidai kwa kutumia lugha zizizo za kwao.

 
“Vita ya lugha ni ya muda mrefu, kama ninyi wataalam wa lugha mtashindwa kusaidia kukuza lugha zetu, kuziandika, basi hazitkuwa na uhai mrefu na zitakufa haraka,” alionya Mkuchika.

 
Alisema wakati nchi za Ulaya zimefanya mapinduzi ya kujikwamua kiasi cha Kiingereza kuwa lugha kuu ya dunia, bado nchi za Kiafrika hazijiamini kuwa lugha zao zinaweza kuiga mapinduzi hayo.

 
Alifafanua kwamba, lugha za Kiafrika zinazovuka mipaka ziwe zinazungumzwa na makabila mbalimbali au zinatumiwa na jamii moja, ni vyombo muhimu vya kuunganisha watu ambao wametenganishwa na ukoloni.

 
“unaweza kuona nchi ndogo kama Iceland inaweza kutumia lugha zake hadi Chuo Kikuu kwenye mambo ya elimu, nchi nyingi za Kiafrika hata zile zenye watu zaidi ya 100 milioni, bado hazijifikirii kutumia lugha zao katika masuala kama hayo, ni jambo la kulifanyia kazi” alisisitiza.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents