Burudani

Anjella aonyesha upendo wake kwa Harmonize, achora tattoo

Msanii wa kike wa muziki Anjella ambaye ni zao la Konde Gang ameamua kuchora tattoo ya jina la bosi wake wa zamani ‘Harmonize’ pamoja na tarehe ya kuzaliwa ’15/03/’ kuonyesha ni jinsi gani anavyokumbuka makubwa aliyofanyiwa katika muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye alikuwa msanii wa kwanza wa kike wa lebo ya Konde Gang kabla ya mapema mwaka huu lebo hiyo kutangaza kuachana naye.

Wadau wa burudani walishangazwa na bosi huyo wa Konde Gang kumuachia msanii huyo bila malipo yoyote tofauti na baadhi ya lebo ambazo msanii ili aondoke anatakiwa kulipa kiasi cha fedha.

Kuondoka kwake kulikuwa gumzo, kwani Konde Gang hawakuweka sababu za msingi na kuibua maswali mengi baada ya muimbaji huyo kwenda kulalamika BASATA kwamba akaunti zake za mitandao bado zinashikiliwa na lebo hiyo.

Hata hivyo BASATA walimaliza sakata hilo baada ya Rais huyo wa Konde Gang kuitwa na kukubali kuachia akaunti hizo huku wadau wakidai kwamba huwenda kukatokea bifu zito baada ya kufikishana kwenye vyombo vya serikali.

Anjella kuchora tattoo kumewapendeza wengi, kwani mashabiki wengi wa muziki walimtaka muimbaji huyo kumshukuru Harmonize kwa kazi kubwa aliyoifanya katika ku-support kipaji chake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents