Habari

Anusurika kifo Ujerumani kwa kupiga saluti ya ‘Hitlergruß’ iliyotumiwa na Adolf Hitler

Mtalii mmoja kutoka Marekani amenusurika kifo nchini Ujerumani baada ya kuambulia kichapo kitakatifu kutoka kwa wazawa kwa kitendo cha kupiga saluti ya ‘Hitlergruß’, saluti iliyokatazwa nchini humo iliyokuwa inatumiwa na Dikteta, Adolf Hitler katika kipindi cha uongozi wake.

Tokeo la picha la nazi salute
Adolf Hitler akipiga saluti ya Hitlergruß kama salamu kwa wafuasi wake wa Chama cha NAZI

Mwanaume huyo mwenye miaka 41 ambaye jina lake lilihifadhiwa kwa sababu za kiusalama alikuwa kwenye bar moja huko mjini Dresden akiwa na familia yake na baadae akaanza kuonesha ishara hizo huku akitaja jina la Adolf Hitler.

“Alikuja na mkewe wakiwa wenye furaha akaagiza kinywaji baada ya masaa mawili akaanza kupiga makelele akiita Adolf… Adolf.. wengi tulijua anamuita mwanaye lakini tukashangaa anaaza kuonesha ishara za chama cha NAZI ndipo watu waliokuwa kwenye Bar wakamvamia na kuanza kumshambulia”, amesema moja ya wahudumu wa Bar hiyo.

Taarifa kutoka kwa maaskari Polisi mjini Dresden wamethibitisha kupokea taarifa hizo huku wakidai Mwanaume huyo ni kweli alionesha ishara ya chama cha NAZI lakini bado hawajafanya uchunguzi wa kutosha kwani bado hajatoka hospitali alikolazwa.”amesema Lutz Milker Msaidizi wa Kamanda mkuu wa Jeshi la polisi mjini Dresden.

“Tumepokea taarifa hizo lakini bado hutajua alikusudia nini mpaka kufanya hivyo ingawaje vipimo vinaonesha alikuwa amelewa hivyo tunasubiri hadi atoke hospitali kwa uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye gazeti maarufu nchini Ujerumani la Sächsische Zeitung zinadai mhalifu huyo aliamuliwa akae chini na wahudumu lakini hakuwaelewa aliendelea kupiga makelele huku akionesha ishara za Chama cha NAZI ndipo watu wenye hasira walipoanza kumshambulia kabla ya polisi kumuokoa.

Tukio hilo lililotokea wikiendi iliyopita linajiri baada ya wiki mbili zilizopita raia wawili kutoka China kukamatwa mjini Berlin kwa kosa la kuonesha na kupiga saluti za Chama cha NAZI na kupigwa faini ya Euro 5,000 kila mmoja na kupigwa marufuku kuitembelea tena nchi hiyo.

Nchini Ujerumani ni kosa kubwa kisheria kuonesha ishara au kupiga saluti za Chama cha NAZI kilichokuwa kikiongozwa na Dikteta Adolf Hitler.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents