Michezo

Arsenal na Man United wapigana vikumbo kumnasa mshambuliaji wa PSG, wengine sokoni

Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito – via Metro)

Edson Cavani

Chelsea sasa wanamlenga mlinzi wa West Ham Issa Diop na wanatazamiwa kutuma dau la usajili la pauni milioni 40 kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 22. (Express)

Manchester United wanaaminika kutaka kumsajili beki wa klabu ya Hellas Verona ya Italia na raia wa Albania Marash Kumbulla, 19. (Star)

Tottenham, Arsenal na Manchester United wanapigana vikumbo kutaka kumsajili beki wa kati Samuel Umtiti, 26, na klabu ya Barcelona inaonekana imedhamiria kumsajili Mfaransa huyo. (El Desmarque – in Spanish)De LigtDe Ligt aliichezea kwa mafanikio Ajax kabla ya kutimkia Juventus

Ajax wanapanga kumrudisha beki Matthijs de Ligt, 20, kwa mkopo licha ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kumuuza Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. (A Bola – in Portuguese)

Chelsea inaonekana haipo tayari kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, huku meneja Frank Lampard akiona mchezaji huyo haendani na kikosi chake. (90min)

Crystal Palace wamekataa kumuuza Zaha kwa vigogo wa Ujerumani Bayern Munich. (Guardian)Wilfred Zaha

Nani kumng’oa Zaha Palace?

Tottenham wamejiunga kwenye mbio za kutaka kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24, huku Milan wakitaka dau la pauni milioni 30. (Guardian)

Spurs hawana mpango wa kutafuta mbadala wa haraka wa kiungo Moussa Sissoko, 30, ambaye ni majeruhi na hatarajiwi kurudi dimbani mpaka Aprili. Hata hivyo, watalazimika kununua kiungo mwengine endapo watawauza Victor Wanyama, 28, na Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)

Arsenal haitarajiwi kufanya usajili wa moja kwa moja mwezi Januari na badala yake watajikita kwenye mikopo. (Goal)

Tetesi Bora za JumatanoOle Gunnar Solskjaer

Kocha Ole Gunnar Solskjaer

Kocha Ole Gunnar Solskjaer amesema wachezaji wengi wa Man United wanacheza kwa ajili ya kesho yao. Kiungo wa England Jesse Lingard, 27 amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake pamoja na kiungo Mserbia Nemanja Matic. Beki wa Mholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22 na beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 25 watamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)

Manchester City wanawania kumsajili winga wa Wolves Mhispania Adama Traore, 23. (Calcio Mercato, via Manchester Evening News)

Wakala wa kiungo wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 32, atafanya mazungumza na Manchester United kuhusiana na uwezekano wa mchezaji huo kuhamia United mwezi huu. (Corriere Della Sera, via Mirror)Ashley Young

Ashley Young

Inter Milan inaripotiwa kumfuatilia nahodha wa Manchester United Ashley Young, 34. (Manchester Evening News)

Aston Villa wako kwenye mawasiliano na Crystal Palace kuhusu kumrejesha mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 29. (Telegraph, via Birmingham Mail)

Villa wamepewa fursa ya kumsajili kipa mkongwe Pepe Reina, 37, kutoka AC Milan. (Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents