Habari

Kasri la kifalme lasikitishwa na maamuzi ya Mwanamfalme Harry na mkewe 

Familia ya kifalme ya Uingereza imesikitishwa na maamuzi ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan kutangaza ‘kuacha’ kujihusisha na shughuli za kifalme.

Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan wametangaza kuachana na shughuli za kifalme

Kasri la Buckingham imehuzunishwa na maamuzi hayo na kusema haikuhusishwa na wala haikuwa na taarifa zozote za awali kuhusu maamuzi ya wanandoa hao.

BBC imebainisha kuwa si Malkia wala mwana mfalme William au waandamizi wengine katika falme walijulishwa hatua hiyo na kwa kwamba uongozi wa juu wa ufalme umepata pigo.

Kasri ya kifalme imesema kuwa suala hili ni gumu sana na wamelipokea kwa mshtuko mkubwa.HARRY NA MEGHAN

Mwandishi wa zamani wa BBC masuala ya kifalme Peter Hunt ameiambia BBC: “Mara nyingi huwa ninapata hofu kutumia neno ‘haijawahi kutokea’ ingawa sina mfano ambao ninaweza kufikiria kusema kuwa familia ya kifalme iliwahi kujisafisha katika jambo kama hili kwa umma.”

Katika maelezo yao, Harry na Meghan walisema kuwa walifikiria uamuzi huo kwa muda mrefu na kufanya maamuzi hayo miezi mingi iliyopita.

Harry na Meghan wamepanga kugawa muda wao kwa nusu kuishi Marekani na nusu Uingereza kuendelea kumtumikia malkia na kujihusisha na shughuli za kifalme.

“Maamuzi hayo yataturahisishia kumlea mtoto wetu katika makuzi ya utamaduni wa kifalme, na kuipa fursa familia kuangalia hatua inayofuata,” walisema wapenzi hao .HARRY NA MEGHAN

Msemaji wa zamani wa malkia Dickie Arbiter alisema kuwa hafahamu ni namna gani wataweza kugeuza mipango yao.

“Hii ni kama ndoto. Kuna suala la usalama: Nani atatoa ulinzi kwao?

“Je, ni nchi gani itawapa ulinzi wa kifalme? Je, ni Canada au? Na nani atalipia?”Mwanamfalme Harry

Hatua hii inakuja baada ya mwezi Oktoba mwaka jana mwanamfalme Harry na mkewe walilalamika kuingiliwa maisha yao kwa kufuatwa na vyombo vya habari kwa kivuli kuwa wanatoka katika familia ya falme.

Katika ukurasa wake wa Instagram,Mwanamfalme Harry na mkewe wametoa utetezi wao kuhusiana na tangazo lao kwamba ,hatua hiyo wameifikia baada ya kuwa na majadiliano ya ndani ya nyumba yao wao wawili kwa miezi kadhaa.

Maamuzi yao yamepingwa kwa kudaiwa kuwa walistahili kupewa idhini ya jambo hilo na kutoa taarifa kabla.

Malengo yao mengine ya kujiondoa katika shughuli za moja kwa moja za kifalme ni kutaka kufanya kazi za kawaida katika kuendesha maisha yao ya kila siku badala ya kutegemea mapato yatokanayo na nafasi zao za kifalme.Mwanamfalme Harry alifunga ndoa na mkewe mwaka 2018Mwanamfalme Harry alifunga ndoa na mkewe mwaka 2018

Ingawaje wamesisitiza kwamba bado wataendelea kumuunga mkono Malkia na ufalme kwa ujumla.

Katika maelezo yake kupitia ukurasa wa instagram mwana mfalme Harry ameomba waruhusiwe kama walivyoamua yeye na mkewe.Mei 6 , 2019, Meghan alijifungua mtoto wa kiume, Archie Harrison Mountbatten-Windsor, ambaye ameingia katika kizazi cha saba cha kiti cha enzi cha ufalme.Mei 6 , 2019, Meghan alijifungua mtoto wa kiume, Archie Harrison Mountbatten-Windsor, ambaye ameingia katika kizazi cha saba cha kiti cha enzi cha ufalme.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kifalme nchini Uingereza wamekaririwa wakibeza hatua hiyo ya Harry na mke wake na kwamba amekuwa akikiuka taratibu kadhaa za namna ya kuishi kama mwana mfalme.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents