Habari

Arsenal watenga donge nono kumbakisha Mesut Ozil

Klabu ya Arsenal ipo teyali kumtengea donge nono la mshahara Mesut Ozil ikiwa ni ofa nono ya mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili aweze kubakia katika klabu hiyo.

Kiungo huyo ambaye ni raia wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu mustakabali wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa sasa, na kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa anaweza kuondoka msimu huu wa kiangazi.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal akikunja kitita cha paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki huku akiongeza na bakshishi.

Arsenal wako tayari kumuongeza zaidi lakini Ozil anaonekana kama bado hayupo tayari akifahamu kuwa anaweza kupata zaidi akienda kwingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents