Burudani

AY asema remix ya Zigo akiwa na Diamond ni funzo kwa wasanii wengine

AY amesema aliamua kufanya remix ya Zigo na Diamond ili kuwapa funzo wasanii wenzake wa ndani.

12509174_10153372908158379_166997376138407366_n

Amesema kufanya remix ya wimbo huo na Diamond ni kuwaaminisha wasanii wa ndani kuwa wanaweza kufanya kolabo zao wenyewe kwa wenyewe na kwenda kimataifa.

“Dhana kubwa ya kufanya kazi na ‘artist’ mwenzangu wa nyumbani ni kuonesha kuwa tunaweza kutengeneza wimbo mkubwa na ukafanya vizuri Afrika nzima bila kutumia artist wa nje,” AY alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM hivi karibuni.

“Hii itasaidia sana ‘kuchange mind’ za wasanii wenzangu. Haikatazwi au kupingwa kufanya na artists wa nje but ‘we wanna show them’ kuwa industry yetu imekuwa kubwa sana, so cha msingi tuunganishe nguvu pamoja,” alisisitiza.

Hadi sasa video ya wimbo huo imeangaliwa kwa zaidi ya mara 340,000 kwenye Youtube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents