MichezoUncategorized

Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeondoka alfajiri ya  leo, tayari kabisa kucheza na mabingwa wa ligi kuu nchini Rwanda timu ya Rayon Sports mchezo wa kirafiki kwa timu hiyo kusheherekea Ubingwa wao siku ya Jumamosi

Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara na mara baada ya mchezo huo, kikosi hicho kitaanza safari ya kurejea nchini Jumapili ijayo.

Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii msimu uliopita, wanaendelea na mazoezi huku ikiwakosa wachezaji wake kadhaa akiwemo nahodha msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, beki Erasto Nyoni, kiungo Salmin Hoza na washambuliaji Mbaraka Yusuph na Shaaban Idd, ambao wako na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Nyota hao wako na Stars inayoshiriki michuano ya Kombe la COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini, ambapo hii leo Stars itajitupa uwanjani kuvaana na Zambia katika mchezo wa hatua ya Nusu Fainali.

Wengine ambao bado hawajawasili ndani ya kikosi cha Azam ni mabeki Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Eneock Atta Agyei (Ghana), kiungo Mcameroon Stephan Kingue na mshambuliaji Wazir Junior, aliyesajiliwa akitokea Toto Africans ya Mwanza.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents