Burudani

Baada ya dhiki faraja, msanii Muchoma wa Rwanda athibitisha hilo

Msanii wa muziki kutoka nchini Rwanda, Muchoma ameendelea kuwa mfano bora kwa vijana waliopo katika mazingira magumu na waliokata tamaa ya kufanikiwa katika maisha.

Akiongea na Bongo5 msanii huyo ambaye pia anafanya muziki wa Singeli ameeleza kuwa licha ya kupitia maisha magumu zamaini haikumfanya akate tamaa katika maisha kwani aliamini ipo siku atafanikiwa.

“Mimi ni yule kijana niliyelelewa kwa umasikini wa chini kabisa, na kwetu tumezaliwa watoto saba na mimi ndiyo mtoto wa kwanza kuzaliwa kwetu , nilitoka kwetu kutafuta maisha nikiwa kijana mdogo sana na nikawa omba omba mtaani na baadaye niwa nafanya kazi za ndani kwenye majumba ya watu, lakini baadaye nikajiingiza katika biashara na nikaenda hadi nchini Uganda .” ameeleza Muchoma

Nyumba ya Muchoma

Kuhusu mafanikio aliyonayo kwa sasa ikiwemo kununua nyumba ya kifahari ya milioni 45 za Rwanda maeno ya Kisenyi nchini humo , Muchoma ameeleza hizo ni moja ya ndoto yake kwani alijitahidi kujinfunza vitu vingi iliasife masikini.

Akaongeza “ Baada ya kuona nimechoka kuwa ombaomba nikaamua kujifunza kunyoa watu nywele maeneo ya Nairobi na baade nikapata kazi ya kuwa kinyozi katika saluni nzuri kabisa ya kifahari, ila peswa za malipo nilikuwa nikizitunga na kisa nikafungua mgahawa wangu ambao ukawa unapanda na kuwa mzuri kabisa.”

“Mafanikio yakazidi na hatimaye nikapata pesa zangu nyingi na nikaenda Marekani, baade nikareje nyumbani (Rwanda) nikawa naendelea na masuala ya biashara na huko ndiko nilipopata pesa za kuweza kujenga nyumba hiyo ya kifahari.”

Lengo la kulezea historia yangu hiyo ni kuwapa moyo vijana wasikate tamaa katika maisha na kuijiona hawezei kubadirisha mambo amesema Muchoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents