BurudaniHabariMahojiano

Baba levo na Mwijaku kimeumana, sababu za wao kutofautiana

Baba levo ameweka wazi kutofautianna na partner wake Mwijaku kuhusu kufanya kazi wote kama ilivyokuwa mwanzo watu walivyozoea kuwaona wakiwa pamoja na kupata madili wakiwa wote.

Baba levo ameeleza ili kujiepusha na matatizo na kutokugombana na wateja wake ameamua kila mtu afanye kazi kivyake kwa kuwa kwenye makampuni kila mmoja anasaini mkataba wake.

Ameeleza sababu nyingine kuwa Mwijaku anamsikiliza zaidi mke wake badala ya kuangalia kazi kwanza hivyo aendelee kumsikiliza mke wake yeye atafanya kazi kivyake.

Mwijaku na Baba levo walikuwa wannafanya kazi pamoja hasa kwenye upande wa promotion za makampuni mbalimbali na walianza kuaminiwa na makampuni mengi zaidi.

Kwenye U-partner wao walitengeneza brand yao waliyoipa jina la MWIBA likimaanisha MWIJAKU + BABA LEVO ili liliwasaidi sanna kuwatangaza.

Moja ya matunda ya ushirikiano wao ni kupata ubalozi kwenye makampuni kama Silent Ocean na GSM lakini pia WASAFIBET na mengine mengi.

Matunda mengine kwa ushirikiano wao nni kwamba walifannikiwa kupata fursa ya kusafiri kweye mataifa kadhaa yakiwemo Qatar kwenye michuano ya Kombe la dunia lakini Dubai na Uturuki.

Kwa ufupi ushirikiano wao ulikuwa na matunda makubwa sana kuwafanya watu wengi kuendelea kuwafuatilia kwani waliziunganisha brand mbili zinazofuatilia Tanzania yaani Baba levo na Mwijaku.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents